Sunday, October 30, 2011

KIDIHESA WAPANIA KUFANYA KWELI KILOMBERO

Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wilaya ya Kilombero (KIDIHESA)
Jana wamefanya kikao cha pili kwenye ukumbi wa Sisimizi bar- ubungo kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri wilaya ya kilombero. Wasomi hao wameunda kamati ili kurahisisha utelekezaji wa majukumu yao. Kamati zilizoundwa ni fedha, mipango na kamati ya maendeleo ya jamii.Mmoja wa wanachama aliyeuzulia kwenye kikao Bw. Prosper Mbwagai alisema tunabidi kuanzisha vyanzo vya biashara kuliko kutegemea ada ya uanachama pekee kwa mfano kuanzisha miradi mbalimbali kama vile uuzaji wa T shirt ili kutunisha mfuko wetu. Mambo waliyoyajadili ni:- 1.Ada ya uanachama Tsh. 10,000/= kwa mwaka
2.Wasomi kutumia taaluma zao kutatua kero zinazowakabili wana kilombero kwa ujumla
3. Kutoa elimu mbalimbali ikiwemo ujasiliamali, mazingira, umiliki wa ardhi
4. Kuitambulisha rasmi katiba yao katika halmashauri ya wilaya ya kilombero
5. Kuunda kamati na kuteua walezi wa KIDIHESA
Umoja huo unaojumuisha wanafunzi wa elimu ya juu wenye asili ya kilombero utafanyika tena mwezi wa kumi na mbili.